Maisha ya kipa wa Liverpool yanavokwenda hivi baada ya fainali.
By Azizi-Mtambo 15
Kipa wa klabu ya Liverpool, Lorius Karius, mwenye umri wa miaka 24, ametishiwa maisha na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya kupoteza fainali ya Uefa dhidi ya Real Madrid.
Watu wasiojulikana walianza kumtishia maisha goli kipa huyo kutumia Mitandao ya kijamii kwa kosa la kupoteza mchezo wao wa fainali.
Karius, alitishiwa maisha pamoja na familia yake kupitia mitandao ya kijami polisi kutoka mjini wa Merseiyeide wamesema kuwa tukio hilo watalichunguza zaidi na kuwa kamati watu hao wanaomtishia maisha goli kipa Huyo.
Karius, alifanya makosa kwenye mchezo huo ambao Liverpool, walifungwa mabao 3-1 goli la Kwanza aliurusha mpira na kumgonga Karimu Benzema, na kuandikia bao la Kwanza Real Madrid, na bao la tatu la Real Madrid, karius, alifanya makosa tena kuipatia bao la tatu Real Madrid, na kutwaa taji hilo.
Mpira ulivomalizika goli kipa huyo alionekana akimwaga machozi na kwenda mbele ya mashabiki wa Liverpool, na kuanza kuonyesha ishara ya kuomba msamaha pia goli kipa huyo aliandika ukurasa wake wa twitter maneno ya kuomba msamaha kwa mashabiki mpaka kwa wachezaji wenzake.
No comments: