Breaking

Mikel Arteta , ana kazi kubwa ya kuifanya.

By Azizi-Mtambo 15

Mikel Arteta, Amezaliwa tarehe 26 march mwaka 1982, akiwa na umri wa miaka 36, ni raia wa Hispania.Arteta, amecheza baadhi za klabu kama Everton,msimu wa mwaka 2005-11, amecheza michezo 162 na kufunga mabao 27 tu . pia amecheza klabu ya Arsenal, msimu wa mwaka 2011-16, amechezea michezo 110, na kufunga mabao 14 tu. Jumla ya michezo amecheza michezo 427, na kufunga mabao 61.



Msimu wa mwaka 2016, aliamua kutundika daluga kucheza mpira na kuamua kuijunga na Manctiy,Msimu wa mwaka 2016/17, Alichaguliwa na kocha wa klabu ya Manchester city, Pep Guardiola, kuwa kocha msaidizi katika klabu hiyo ndo kwanza ana msimu wa pili katika benchi la ufundi kwa ngazi ya ukocha msaidizi.



Baada ya kocha klabu ya Arsenal, Arsene Wenger, kutangaza kuachana na klabu hiyo mzee Wenger, aliyedumu katika klabu hiyo kwa takribani miaka 22, toka Mwaka 1996-2018,na kuacha historia aliyetwaa ubingwa Msimu wa mwaka 2002-03, kutoa ubingwa bila ya kupoteza mchezo hata moja(invisible).




Arteta, amehusishwa kuiongoza Arsenal, msimu ujao na akipewa nafasi kubwa.



Ni jina linalopewa nafasi kubwa ya kuvaa viatu vya Arsene Wenger, akionekana kubwa chaguo mbele ya Ivan Glazidiz,je ni wakati sahihi kwake?



Kutambua yote haya kwa kuondoka kwa Wenger, team inaanza mfumo mpya wa uendeshaji kocha atabaki kama kocha na sio Manager, kama Wenger, hii ni kumpunguzia mamlaka kubwa kwake kazi hizo zitafanyiwa na wengine.



Arteta, akiwa kama pendekezo kufanya hivyo huyo hawezi kuwa kama Wenger, hapana?anakuta mfumo mpya zaidi mabao pengine sio rafiki na kudumu kwa muda mrefu pasipo na mafanikio.



Arteta, hana rekodi kubwa katika ngazi ya ukocha tangu astafuu alikuwa Manchester city, kama kocha msaidizi tu wa Pep, pengine ilikuwa ni mipango yake  kuongeza ujuzi zaidi japo ni mapema kusema atafanya nini anaweza asiwe chaguo baya kama akipewa mda wa Hispania, wana viashirio vya ukocha wazuri.




Mafanikio ni majaaliwa tu aina maana waliofeli hawajui?hapana bali ni mipango inahitajika ya hali ya juu.

No comments:

Powered by Blogger.