Radja Nainggolan, atoa uwamuzi baada ya kuachwa na timu yake ya taifa kuelekea michuano ya kombe la dunia.
By Azizi-Mtambo 15
Kiungo wa klabu ya Asroma, na timu ya taifa Ubelgiji,Radja Nainggolan, ameachwa katika kikosi kitakachoenda michuano ya kombe la dunia hapo mwezi ujao nchini Urusi.
Kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji ,Roberto Martinez, amemuacha mchezaji huku akisema ni tatizo la kiufundi ndo limemfanya amuache.
Nainggolan, ambaye pia alishindwa kupata nafasi ya awali katika michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Brazil, Mwaka 2014, ni mshangao mkubwa kushindwa kumchagua tena katika kikosi hicho cha Ubelgiji, kwa kuzingatia Marouane Fellaini, na Axel Witsel, wao wawili wanabaki kuwa wachezaji muhimu katika timu ya taifa licha ya kuwa na viwango vya hali ya chini katika klabu zao wanazochezea.
Martinez, anaendelea na mfumo wake wa 3-5-2, na 3-4-3, je unadhani yupo sahihi kumuacha kiungo huyo?
Nainggolan, ametangaza kustafu soka kwa ngazi ya taifa mara ya mwisho kuchezea taifa hilo ilikuwa Mwaka 2016, kule nchini Ufaransa,katika michuano ya Euro.
No comments: