Fernando Santos asema haya kuelekea mchezo wao wa hatua ya mtoano kombe la dunia.
By Aziz-Mtambo 15.
Kuelekea mechi ya hatua ya mtoano kwenye fainali za kombe la dunia. Kocha wa Portugal, asema yafuatayo.
Kocha wa timu ya taifa Portugal ,Fernando Santos, amesema kuwa mchezaji wake bora duniani Cristiano Ronaldo, hawezi kuwafunga Uruguay, Peke yake inahitaji timu nzima ijitume zaidi ili ipate matokeo mazuri.
Cristiano Ronaldo, ambaye katika fainali za kombe la dunia za Mwaka huu ameshafunga mabao 4 na pia kocha huyo amesema timu yake inaweza kushinda bila ya Ronaldo, huku akisema tuliwafunga Ufaransa, fainali ya kombe la Ulaya Mwaka 2016, bila ya Ronaldo, aliyeumia katika pambano hilo na kutolewa kipindi cha Kwanza.
"Tunahitaji tucheze kama timu na kama Ronaldo, akicheza kwa uwezo wake tutapoteza,".kocha huyo alihojiwa huko nchini Urusi.
"Tunahitaji kuwa na nguvu Kama timu na pia Uruguay, ni timu yenye wachezaji bora,".
"ni ngumu kucheza kucheza Ronaldo, peke yake hata mchezo wetu dhidi ya Spain, alifunga mabao matatu tulicheza kitimu,".
huku akisema anatoa onyo kuelekea mchezo huo akisema Uruguay, nyuma katika safu ya ulinzi wana beki imara ikiongozwa na Diego Godin, na katika safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Cavani, na Suarez.
"Wana beki ambaye anachezea Athletico Madrid, na msimu huu ametwaa taji la Europa, na wana viungo wawili moja anachezea Juventus, mwengine Inter Milan,".
'Wana washambuliaji moja anacheza Paris Saint Germain, mwengine anachezea Barcelona, na wote wameshinda mataji katika timu zao,".
"na imani timu yangu itacheza katika kiwango bora kama itakavocheza Uruguay,".
No comments: