Uchambuzi mechi kati ya Iran, dhidi ya Portugal.
By Azizi -Mtambo 15.
Leo jumatatu, kutakuwa na mchezo wa kundi B Portugal, dhidi ya Iran, mchezo huo utapigwa katika dimba la Mordovia Arena.
Iran, kuelekea mchezo wao wa leo watamkosa beki wao Ehsan Hajsafi, aliyepata majeruhi katika mchezo wao dhidi ya Spain, na nafasi yake itachukuliwa na Milad Mohamed.
Kocha wa Iran, Carlos Queiroz, akiongelea mchezo wao dhidi ya Portugal.
"baada ya kucheza michezo miwili tumecheza vizuri na tumekuwa vizuri Sana,".
"bado tuna nafasi ya kufuzu kwenda hatua nyengine,".
"Portugal, wana kikosi kizuri wana wachezaji bora duniani,".
Kocha wa Portugal, Fernando Santos, akiongelea mechi yao ya leo.
"Iran, michezo yao miwili wamecheza vizuri sana wanajua kujipanga katika eneo la ulinzi,".
"wanatumia mpira mirefu wana washambuliaji bora katika ufungaji,".
Tukumbuke.
Mara ya mwisho Iran, na Portugal, walikutana Mwaka 2006.Portugal, alishinda mabao 2-0 .magoli yao yalifungwa na Deco, na Ronaldo.
Vikosi vinavoweza kuanza leo.
Iran. Beiranvand, Haji Safi, Pouraliganji, Rezaien, Hosseini, Ezatolahi.
Portugal. Patricio, Pepe, Fonte, Guerrero. Soares, Carvalho, Mountinho, Silva, Mario, Guedes, Ronaldo.
No comments: