Breaking

Didier Deschamp, anahitaji pongezi.

By Azizi -Mtambo 15.

Baada ya jana Ufaransa,  kutinga fainali katika fainali za kombe la dunia kwa kumfunga Belgium,  bao 1-0 hakuna mtu au niseme watu wachache duniani walimpa nafasi ya kufanya vizuri na wengine walikuwa wakizipa nafasi timu kama Brazil, Argentina, Ujerumani, Spain, leo hi timu hizi ambazo zilikuwa zimetawala soka kwa hivi karibuni leo zipo wapi? mie na wewe majibu tunayo. tusiishi kwa kukariri au kwa mazoea mpira una matokeo yake leo hi tumepata jibu sahihi?.

Mara ya mwisho Ufaransa kutowa ubingwa wa dunia ilikuwa Mwaka 1998, kule nchini Ufaransa,  kulikuwa na kizazi cha dhahabu chini ya kocha wao Armie Jacquet,  walimfunga Brazil,  mabao 3-0 tena kwa aibu shukrani kwa mabao mawili ya Emanuel Petit,  na Zinedine Zidane,  Ufaransa, aliweka rekodi ya kuwa timu ya Kwanza kushinda mabao 15 katika fainali za kombe la dunia rekodi hiyo ilikaa muda mrefu mpaka Ujerumani, alipokuja kuivunja Mwaka 2014 wao walifunga mabao 18.

Kikosi cha Mwaka 1998, kilikuwa kizazi bora kabisa kikiongozwa na watu kama Thienry Henry,  Zinedine Zidane,  Fabian Barthez, Patric Viera,  maisha yanaenda kasi kweli leo hi wameshatundika daluga wengine.

Fainali za kombe la dunia kule nchini za Mwaka 2002 Japan Ufaransa,  alitolewa hatua ya makundi tena cha ajabu zaidi alifungwa na Senegal,  ya kina D. Cisse,  kikosi kilikuwa na wachezaji waliotwa ubingwa Mwaka 1998, Zinedine Zidane,  Thienry Henry,  lakini walikosa hamasa.

hili gundu au janga la kutoka bingwa mtetezi kwenye makundi kulianzia kwa Ufaransa,  na iliendelea mpaka kwa wengine kasoro kwa Brazil,  wao waliishia hatua ya robo fainali Mwaka 2006, kule nchini Ujerumani.

Fainali za Mwaka 2006 kule nchini Ujerumani,  walienda na kizazi chao walikuwa na wachezaji wale wale lakini baadhi waliongezeka wapya jahazi lao liliongozwa na Zidane, Henry,  na wengineo. Kwenye hatua ya makundi walifunga mabao mawili tu hatua ya 16 bora walimfunga Spain mabao 3-1 na robo fainali walimfunga Brazil, bao 1-0  na nusu fainali walimfunga Ureno 1-0 kwa jumla walifunga mabao sita katika fainali hizo. lakini walipoteza fainali dhidi ya Italy,  kwa mkwaju ya penalti 5-3 huku penalti ya Trezquet,  kwa upande wa Ufaransa ilikula besela na kuwapelekea kilio Ufaransa.



Ufaransa walionekana kutawala mchezo huo kwa kiasi kubwa eneo la kati likiongozwa na Zidane, walionekana kuwa watashinda kutokana na Italy,  kucheza Soka la kujilinda zaidi.Zidane alionyeshwa kadi nyekundu na kutolewa nje kwa kosa la kumpiga kichwa mchezaji wa Italy,  Materezi na kutolewa kwa Zidane,  kuliwafanya Italy,  kurudi mchezoni zaidi.


Turudi kwenye tukio la Zidane.

Baada ya kupewa kadi nyekundu. alitangaza kustafu soka kwa ngazi lakini mwenye alisema kuwa nilifanya vile kwa sababu ya Materazi alimtukana Dada yake siri ya Zidane, na Materazi wanaijua wenyewe?.



Fainali za Mwaka 2010 kule nchini South Africa,  Ufaransa, waliishia makundi na kutolewa kwa aibu kubwa sana Thienry Henry,  alicheza dakika chache tu.


Mwaka 2012 timu hiyo alipewa Didier Deschamps,  alitengeneza timu huku alikuwa akitegemea wachezaji chipukizi kwenda fainali za Mwaka 2014 kule nchini Brazil,  kulikuwa na wachezaji wadogo kama Griezmann,  Varane,  Valbuena,  wachezaji wakongwe walikuwa baadhi alifanya mchanganyiko wakongwe walikuwa Evra, Benzema, waliishia hatua ya robo fainali walitolewa na ujerumani,  walifungwa bao 1-0.kwenye fainali hizi walifunga mabao 8 tu.




Fainali za Mwaka 2018 imekuwa moja ya timu bora mpaka sasa leo hi wametinga fainali wamefunga mabao 8 ni idadi ya mabao ambayo wamefunga Mwaka 2014 kule nchini Brazil.



Didier Deschamp,  ndo kocha ambaye ameiongoza Ufaransa,  kushinda michezo mingi zaidi toka alivochukua timu hiyo Mwaka 2012.

Tuangalie makocha hao .

Armie Jacquet, michezo 53 ushindi 34 sare 16 kupoteza 3.

Raymond Domenech, michezo 79 ushindi 41 sare 24 kupoteza 14.

Didier Deschamp michezo 82, ushindi 52 sare 15 kupoteza 15.

No comments:

Powered by Blogger.