Breaking

Kilichowaponza England, juu ya Croatia

By Azizi -Mtambo 15.

Croatia, yatinga hatua ya fainali kwenye fainali za kombe la dunia za Mwaka 2018 badaa ya kuwafunga England, mabao 2-1.mchezo huo ulikuwa mchezo wa kuvutia zaidi na timu zote zilianza kwa kasi zaidi kushambuliana.


England kama kawaida yako kutokana mfumo wao 3-5-2 kwenye mashindano haya wamekuwa na faida kubwa kutokana wachezaji wao warefu alafu wanacheza mpira mirefu kuanzia nyuma mpaka mbele mpaka sasa kati ya mabao 11 mabao 9 wamefunga kwa njia ya mipira ya kutenga (set pieces).  England, walianza kutangulia kwenye mchezo wa leo kumbe Croatia, walikuwa wana wasoma mbinu zaidi za uchezaji.

Kipindi cha Kwanza waliweza kumzuia Modric,  wakiamini huyo ndo silaha yao  kubwa zaidi kwenye kuanzisha mashambulizi utawezaje kumzuia Modric alafu ukamuachia Ivan Rakitic? Jibu linakuja England,  walikuwa wana kiungo mkabaji moja tu katika eneo la kati ambaye hawezi kufanya kazi mbili kwa kati moja amzuie Modric,  na kumzuia Rakitic? lbda kwa mawazo yangu mie Southgate, angemuanzisha nje Lingerd,  na Dier, angeingia kikosini kumsaidia Henderson,  kukaba upande wa pembeni kumpunguza kasi Rakitic.


hata ukiangalia kwenye umiliki wa mipira alikuwa anaongoza Croatia,  kwa sababu alikuwa na aina ya viungo ambao wana uwezo wa kukaa na mpira na kupunguzisha plesha kutoka timu pinzani? Je England, wana kiungo wa aina hiyo jibu hapana ukifuatilia watakwambia Rahimu Sterling, Sterling, anacheza nyuma ya Kane,  kama no 10 sawa lakini sio mzuri kwenye kukaa na mpira na kupunguza plesha ya wapinzani? England walifeli eneo la kati.


Ukiangalia,  baada ya kusawazisha kwa Croatia,  kupitia Perisic,  England walipaniki na kutoka mchezo Croatia ndipo alipotumia uwazi huo kutengeneza nafasi za mabao niseme tu England, hawajatolewa bali wamejitoa wenyewe?


Unamtoa Henderson,  unampa nafasi Dier,  kwa shindwa Henderson,  ataweza Dier?jibu linakuja kuwa mwalimu Ange wachezesha wote wawili eneo la Kati wangefanikiwa battle kwenye eneo la kiungo? Unamtoa Sterling, unamuingiza Rashford,  akacheze no 10 kwely?wakati Rashford,  ni mzuri akitokea pembeni.


Lovren, kuwa nilisema anamfahamu vizuri Kane, na ameweza kumtonya beki wenzake wa kati kuwa Kane ni hatari unajitahidi usimpe nafasi kwenye mipira ya vichwa.

Maguire, Stones,  leo mumecheza kawaida sana labda niseme kuwa muliwazarau wakina Mandkuzic,  na Perisic,  kwa kuwa ni wazee.


Takwimu zinaonyesha kuwa Croatia wapo juu zaidi ya England.

Croatia.                          England

Shots 4.                             Shots 1.

Ball possess 56.               Ball posess 44.


Corner 5.                              Corner 4.

Pass kwa jumla 501.           335.

Pass za usahihi 78.           74.


Croatia, alicheza kwa discipline,  na alistahili ushindi. eno la kiungo walimiliki kama ipasavyo.


No comments:

Powered by Blogger.