Croatia, dhidi ya Ufaransa hapatoshi.
By Azizi -Mtambo 15.
Croatia, jana amefanikiwa kutinga hatua ya fainali katika michuano ya kombe la dunia kwa mara ya Kwanza katika historia ya kombe la dunia kwa kuwafunga wajuu wa Malkia Elizabeth, (England) mabao 2-1.mara ya mwisho Croatia, kucheza hatua kama hi ilikuwa Mwaka 1998, kule nchini Ufaransa, tena kizazi hicho cha kina Slaven Billic, Davor Sucker, Niko Kovac, Mario Stanic, tena waliishia hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-1 tangu kizazi hicho kilivofanya hivo imepita takribani miaka 20 je kizazi cha sasaivi cha kina Modric, Perisic, na Mandkuzic, kina weza kutengeneza rekodi yao ya kutwaa ubingwa wa dunia.
Jibu linawezekana Croatia, ya Mwaka huu imekuja tofauti imekuwa moja ya timu ambazo watu wengi walikuwa haipi nafasi ila ukwely unapaki pale pale wanacheza kwa kujituma zaidi na kutafuta matokeo katika michezo yao miwili ya mwisho wametokea nyuma na kupata ushindi? Jibu linakuja kuwa ni moja ya wapambani wakiwa uwanjani.
Tukiangalia mara ya mwisho kucheza hatua kama hi timu ya Croatia, eneo la kati kulikuwa na wachezaji walikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira Aljosa Asanovic, Zvonimir Boban, Mario Stanic, wamekuwa utamaduni zaidi timu yao kuwa bora eneo la kati ndo huwa tuna amini zaidi katika michezo wa mpira wa miguu kuwa timu bora inaanzia kujengwa eneo la Kati. Leo hi eneo la kati wana wachezaji pia wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira Modric, Rakitic, Rebic, hawa wachezaji wamekuwa tishio zaidi eneo la Kati kuanzia kwenye ukabaji mpaka kwenye ushambuliaji na kutengeneza nafasi.
Ufaransa, ni moja ya timu bora katika fainali za Mwaka huu pia ukiangalia wana mafanikio kwa ngazi ya taifa mara ya mwisho kutwaa taji hili ilikuwa Mwaka 1998, kule kwao nchini Ufaransa, walikuwa na kizazi cha dhahabu zaidi kumbuka pia Ufaransa, alimtoa Croatia, hatua ya nusu fainali kwa kumfunga mabao 2-1 Ufaransa, ilikuwa ikiongozwa na Didier Deschamp, Zinedine Zidane, lakini leo hi hawapo katika kikosi amebakia mtu moja ambaye ni kocha wao wa sasa Didier Deschamp, maisha yanaenda kasi sana.
Ufaransa, mara ya mwisho alicheza fainali ilikuwa Mwaka 2006 , kule nchini Ujerumani, na alipoteza dhidi ya Italy, kwa mikwaju ya penalt 5-3.leo Ufaransa, kimekuja kizazi kipya cha kina Kylian Mbappe, Paul pogba, Ng'olo Kante, kuna utofauti kidogo Ufaransa, ya Mwaka 1998, na Ufaransa, ya sasa utofauti unakuja eneo la kati Ufaransa, ya 1998 kulikuwa na viungo wengi wabunifu ambao wana uwezo wa kupiga pass fupi fupi ndefu kukaa na mpira Ufaransa hi ya sasa wana mtegemea Paul Pogba, ni moja ya wachezaji bora ambae sio mbunifu bali ana sifa moja tu ya kupiga mpira mirefu zaidi.
Fainali kati ya Croatia, dhidi ya Ufaransa, itakuwa mchezo wa kuvutia kwa sababu ubora wa timu zote mbili zimekuwa zikicheza kwa discipline ya hali ya juu zaidi.Croatia ni moja ya timu ambao ina mastaa wachache lakini wanajua kutumia zaidi nafasi watakazo zipata.
Croatia, katika eneo la ushambuliaji wana wachezaji wenye experience ya hali ya juu Mario Mandkuzic, Ivan Perisic, wote wanacheza katika ligi bora duniani safu ya ulinzi ya Ufaransa, ina kazi kubwa ya kufanya kuwazuia.
Lovren, na Vida, wana kazi kubwa ya kumzuia Kylian Mbappe, ambae amekuwa mchezaji balaa zaidi katika safu ya ushambuliaji ya Ufaransa, amekuwa akitengeneza nafasi kutokana na umahili wake mkubwa uwanjani.
Kuna mtu moja kanitonya na kunihambia pembeni mechi ya fainali itaamuliwa zaidi eneo la kiungo kutokana na uimara wa timu hizo eneo la kiungo? Tuanze kwa Ufaransa, wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-3-3 katika kuna Kante, Pogba, na Matuidi, Pogba, amekuwa akicheza akitiokea pembeni zaidi lakini sio mbunifu zaidi sifa ya Pogba, ni kupiga mirefu tu? Je ataweza kufanikiwa mbele ya Rakitic, ambae ana uwezo wa kukaba na kukaa na mpira.
Kante, ataweza kumzuia Modric, ambae amekuwa ndo chachu ya mafanikio eneo la kiungo jinsi ya kumzuia Modric, ni kufanya nae battle au kutembea nae ili asipate nafasi ya kutengeneza mashambulizi au hata kupiga mashuti.
No comments: