Marcos Alonso uso kwa uso na rungu la chama cha soka cha fa.
Beki wa klabu ya Chelsea Marcos Alonso,amefungiwa michezo 3 na chama cha soka cha FA kwa kosa la kumchezea rafu mshambhuliaji wa klabu ya southampton jumapili iliyopita beki huyu alimchezea vibaya mshambhuliaji huyo wakati wanagombania mpra.
Mwamuzi aliyecheza pambano hilo Sikh ya jumapili tarehe 15 mwezi huu alishindwa kuliona tukio hilo na baada kamati ya chama cha soka nchini uingereza kilirudia marudio ya mkanda wa picha na kutoa adhabu hiyo Kali kwa mchezaji huyo.
Chelsea michezo huo alitokea nyuma kwa kufungwa mabao 2_0 na kushinda 3_2 shukrani kwa mabao yaliyofungwa na Oliver giroud aliyetokea sub na kupachika mabao 2 na lengine akifunga mshambhuliaji wao Eden hazard,.
Alonso atakosa michezo kama ifuatavyo michezo dhidhi ya Burnley, nusu fainali ya kombe la FA dhidhi ya Southampton ,na mchezo wao wa ligi dhidhi ya Swansea city msimu huu beki huyu amekuwa tegemeo kwenye klabu hiyo amefunga mabao 6 ndo beki mwenye magoli zaidi barani ulaya pia ameingia kwenye kikosi bora cha ligi kuu msimu huu.
No comments: