Mzimu wa Simba na Yanga yaitesa Azam fc.
Kila nikitazama klabu ya Azam Fc kichwa kiunauma au sipati majibu Azam ndo team peke yenye kila kitu hapa nchini kwetu inapesa,imetokea katika familia ya utajiri ,INA uwanja wake binafsi unaitwa Azam complex upo chamazi, INA basi la kisasa lenye choose ndani,television, kuna kiyoyozi,sijui tatzo kubwa nin kinaikuta hii timu?ina miundo mbinu mizuri mno ya kuvutia kwenye soka letu.
Azam inashndwa kufikia kasi ya timu kongwe hapa nchini kwetu kama Simba,Yanga wakati hizi timu zinategemea wanachama mbali mbali,kwenye uendshaji wa timu zao?
Mwaka 2012 Azam ndiyo ilianza vizuri kwa kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara .mwaka unaofuatiwa 2014 walitwaa ubingwa wa kombe hilo kwa kuweka rekodi ya kutopeza mchezo hata moja .
Mwaka 2015 ikatwaa kombe la kagame kwa kuweka rekodi ya kutopeza mchezo hata moja na kutoruhusu wavu wake kuguswa.
Msimu huu teyal azam ashacheza michezo 24 na kukusanya alama 45 akiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara .mwendelo wake mbaya sana.
Msimu huu ashatolewa kwenye kombe la fa dhidi ya Mtibwa sugar katika uwanja wake wa nyumbani azam complex kwenye ligi kuu hawana chao.wanabaki kukamilisha ratiba.
Azam hivi karibuni wameondokewa na mastaa wao kibao kwenye timu hiyo John Bocco alkuwa aina ya mshambhuliaji tegemezi kabisa kwenye safu yao ya mshambhuliaji akiwa yeye na muivory cost Kipre tchetche hawa wachezaji waliondoka kwa sababu walishndwa kuelewana na baadhi ya viongozi wa timu hiyo kwenye suala la mikataba mchezaji lazma umbane kwenye mikataba na sio kumuacha Uhuru zaidi huu ni uzembe ambao wamekuwa wakiufanya hivi karibuni bado akaondoka beki wao kati pascal wawa ,pamoja na shomary kapombe kwa swala hilo hilo me nafkri azam kwenye swala la mikataba yao wameshndwa kuendana na kasi hiyo.
Teyal kuna taarifa zinasema kwamba mwisho wa msimu huu watamuondoa kocha wao Mromania Artistic cioba,kutokana na mwendo wake mbovu na kumchukua kocha wa singida Hana van der pluijm, kama watafanya hivo watakuwa wamelamba dume.
No comments: