Pep Guardiola amebakiza kuvunja rekodi hizi tu epl.
By Azizi Mtambo 15
kocha wa klabu ya Manchester city Pep Guardiola,akiwa teyali ameshatangaza ubingwa wa ligi kuu England bado kilichobaki ni kukabidhiwa kombe lake msimu huu.
Guardiola anahitaji kuvunja rekodi zifuatavyo ili atengeneze ufalme wake katka ligi kuu England.
Point nyingi.
Rekodi ya kwanza ni ile ya point 95,iliyowekwa na Chelsea msimu wa mwaka 2004/05 rekodi hiyo imedumu kwa takribani zaidi ya miaka 13 sasa lakini Guardiola ashatangaza ubingwa zikiwa zimebakia michezo 4 kuisha kwa sasa akiwa na alama point 90 Guardiola ana asilimia kubwa ya kuvunja rekodi hi iliyowekwa na Jose mournho msimu wake wa kwanza akiwa na Chelsea city mpaka sasa imeshinda michezo 29 ,sare 3 na kupoteza 2 imebakisha michezo 4 kuvunja rekodi ya Jose akiwa na Chelsea na kutengeneza yake mechi zinavofuata atacheza na Westham, kisha Huddersfield, na brightoni,.
Kushinda mechi nyingi.
Hi rekodi ambayo iliwekwa na Chelsea msimu wa mwaka 2016/17 chini ya Muitaliano Antonio Conte,kushinda michezo 30 rekodi hi ambayo pep anahitaji kuvunja zaidi na kuweka take mpaka sasa city wameshinda michezo 29 wanahitaji kushinda michezo 2 na kuweka rekodi yao.
Kushinda mechi nyingi ugenini.
Hi rekodi inashikiliwa na Chelsea kushinda michezo mingi ugenini msimu wa mwaka 2004/05 Chelsea alishinda michezo 15 ugenini cty mpaka sasa wameshinda michezo 14 wanahitaji michezo 2 kuvunja rekodi hiyo na kutengeneza yao.
Kufunga mabao mengi.
Hi rekodi nyengine iliyowekwa na Chelsea ambayo city imepania kuvunja iliwekwa msimu wa mwaka 2009/10 chini ya Carlo Ancelloti ,ilifunga mabao 103 na kubeba ndoo cty mpaka sasa anahitaji mabao 11 kutengeneza rekodi yao.
Pengo la point kubwa.
Rekodi ndio inashikiliwa na Manchester united msimu wa mwaka 1999_2010 chini ya babu Sir Alex Ferguson ,walishinda makombe matatu na kubeba ndoo ya epl kwa tofauti ya point 18 utd alkuwa na point 91 huku arsenal akiwa na point 73 rekodi hiyo imedumu kwa takribani miaka 19 kubeba kombe tofauti ya point 18 katika michezo 4 Manchester city anahitaji kushinda yote minne huku akiomba utd atoe droo na kupoteza
No comments: