Yanga yakubaliana kiainaina kuwa simba ndo bingwa msimu huu.
By Azizi Mtambo 15
Mchezo wa watani wa jadi uliyomalizika hivi awali Simba alikuwa nyumbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kumkaribisha mabingwa wa kihisitoria Yanga afrika katika mchezo wa ligi kuu vodacom premier league.
Mchezo huu ulianza kwa kasi mno huku yanga wakitegemea mipra mirefu kutokana na mshambhuliaji wao mahiri Obrey Chirwa, lakini umakini wa safu ya ulinzi ya simba ilifanikiwa kumbana na kutompa nafasi mpra uliendelea lakini katika mchezo huo simba walionekana kutawala zaidi mchezo huo kwenye eneo La kati huku yanga wakicheza mpra wa kujilinda zaidi.
Dakika ya 37 beki wa simba sport klabu Eransto Nyoni anaipatia bao la kuongoza kupitia mpra wa adhabu uliopgwa na Shiza kichuya na kumkuta beki huyo kufunga bao hilo kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili mpra ulianza kwa kasi mno huku yanga ikionekana kutafuta bao la kusawazisha lakini mipango yao ilishindwa kuendana na matarajio baada ya beki wa klabu ya yanga Hassan Kessy,kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 48 kipindi cha pili.
Baada ya ushindi wa Leo simba imekusanya jumla ya alama 62 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Azam akiwa na alama 49 huku yanga akiwa nafasi ya 3 na alama 48 lakini yanga ana viporo viwili akishinda viporo hivo atarudisha matumaini ya kuwania nafasi ya pili.
Nahodha wa yanga Kelvin Yondani huenda akakutana na adhabu Kali kutoka kwa shirikisho la soka Tanzania TFF,kwa kosa la kumtemea mate beki wa simba Asante kwasi tukio hilo mwamuzi aliyecheza mchezo huo hakuliona lakini tuxubiri ripoti kwa kamisa na tuone hili swala la nahodha huyo watalichukuliaje.
Simba inahitaji alama 5 ili kutangaza ubingwa msimu huu huku akiwa amebakia na michezo 4 tu.
Simba vs Ndanda fc(nyumbani).
Singida united vs simba(ugenini).
Simba vs kagera sugar (nyumbani).
Simba vs majimaji(nyumbani)
Ndo michezo ya simba iliyobaki msimu huu anahitaji ashinde michezo tu ili atangaze ubingwa msimu huu amekaa takribani miaka 6 bila ya taji.
Yanga amebakiwa na michezo 6 mpaka sasa ligi kufikia tamati.
Yanga vs Mbao fc(nyumbani)
Mtibwa sugar vs yanga(ugenini)
Mwadui vs yanga(ugenini)
Prison vs yanga(ugenini)
Yanga vs Ruvushooting(nyumbani)
Yanga vs Azam(nyumbani)
Hiyo ndo michezo ya yanga kabla ya kufikia tamati ligi kuu vodacom .
No comments: