Roberto Firmino amwaga wino liverpool.
By Azizi Mtambo 15
Mshambhuliaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino, mwenye umri wa miaka 26 amesaini mkataba mpya na klabu ya Liverpool mkataba huo utamfanya mchezaji huyo abaki klabuni hapo mpaka mwaka 2023.
Mshambhuliaji huyo aliyejiunga na klabu ya Liverpool akitokea Hoffeinhm ya ujeruman mwaka 2015.
Mkataba wa hapo awali alikuwa akilipwa kitita cha paundi milioni 12,0000 kwa wiki zaidi ya wachezaji wengi wa Liverpool zaidi ya hata Mo Salah,.
Mkataba wake wa sasa analipwa kitita cha paundi million 18,0000 ni sawa na tsh million 564 kwa wiki hata kuwa mchezaji anayepokea pesa nyingi huku akiungana na beki wake Van Djik.
Mpaka sasa firmino amefunga mabao 10 kwenye mashindano ya uefa msimu huu na pia timu yake ipo kwenye nafasi nzuri ya kutinga fainali ya uefa msimu huu.
Firmino mpaka sasa amefunga mabao 15 msimu huu kwenye ligi kuu England na kutoa assist 7 katika ligi hiyo.
Msimu wake wa kwanza 2015/16 alichezea michezo 37 na kufunga mabao 10 kwenye ligi kuu England.
Msimu wake wa pili mwaka 2016/17 alichezea michezo 35 na kufunga mabao 11.
Msimu wake wa tatu amecheza michezo 35 na kufunga mabao 15.
No comments: