Arjean Robben, amwaga wino Bayern munch.
By Azizi Mtambo 15
Mshambhuliaji wa klabu ya Bayern munch, Arjean Robben, mwenye umri wa miaka 34, ameongeza mkataba na klabu yake Bayern munch, mchezaji huyo mkataba wake ulikuwa una maliza mwisho wa msimu huu.
Mchezaji huyo ameongeza mkataba wa miaka moja na miamba hiyo ya Ujerumani, na utamfanya abaki klabuni hapo mpaka mwaka 2019.
Robben, ambaye amechezea michezo 189, ligi ya Ujerumani, maarufu kama Bundesliga, na kufunga mabao 95, katika ligi hiyo.
Pia ameshinda makombe 17, akiwa na Bayern munch, ameshinda kombe la ligi kuu Mara 7, mwaka 2009/10, 2012/13 2013/14, 2014/15, 2015/16, 2016/17, na mwaka 2017/18, pia ametwaa kombe la UEFA Mara moja mwaka 2013, na pia kombe la Ujerumani, Mara 4 mwaka 2009/10, 2012/13, 2013/14,na 2015/16, pia ameshinda kombe la klabu bingwa Mara 1mwaka 2013, pia ametwaa kombe la ngao ya hisani mara 4 ,mwaka 2010/11, 2012/13, 2016/17, 2017/18,.
Pia mwaka 2013, alifunga bao la ushindi kwenye fainali ya UEFA dhidhi ya Borrusia Dortmund na kutwaa taji hilo .
No comments: