Breaking

Buffon atangaza kuachana na soka mwisho wa msimu huu.

By Aziz-Mtambo 15


Nahodha wa klabu ya juventus, Giunluigi Buffon, ametangaza rasmini kuwa ataachana na soka mwisho wa msimu huu goli kipa huyo aliyedumu na klabu hiyo kwa takribani miaka 17, sasa ametangaza kuachia ngazi rasmini.





Buffon, aliyejiunga na klabu ya juventus, Mwaka 2001, akitokea palma kwa kitita cha paundi million 30 na kuwa goli kipa ghali duniani rekodi hiyo iliyodumu kwa takribani miaka 17, na ilikuja kuvunjwa na goli kipa wa klabu ya Manchester city Ederson Moreas, kwa kitita cha paundi million 35, akitokea Benefica nchini Ureno.




Buffon, ameshinda mataji 23, kwa ngazi ya soka makombe 9, ya ligi kuu Italy maarufu series A, makombe 5 coppa italia, 6 super coppa Italia, na 1 uefa, kombe la dunia 1, na 1 kombe la series B.



Buffon, amecheza michezo ya ligi kuu Italy, 508. pia amechezea michezo 176 timu ya taifa ya Italy.

No comments:

Powered by Blogger.