Buffon uso kwa uso na shirikisho la UEFA
By Azizi Mtambo 15
Nahodha na goli kipa wa Juventus, Gianluigi Buffon, amekumbana na adhabu kutoka shirikisho la soka UEFA, goli kipa huyo ambaye aliotolewa nje kwa kadi nyekundu katika mchezo wa robo fainal ya uefa, kati ya Real Madrid dhidhi ya Juventus.
Mchezo huo uliopigwa mwezi uliopita katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu, hatua ya robo fainal michuano ya uefa msimu huu.
Goli kipa huyo mwenye umri wa miaka 40, alionekana kutoheshimu maamuzi ya mwamuzi aliyechezesha pambano hilo Michael oliver huku akimshutumu kwa kumfokea baada ya kuwapa real Madrid penalti dakika za mwisho.
Mchezo huo ulishia kwa real Madrid, kufungwa mabao 3_1 na kupita kwa jumla ya mabao ya ugenini 4_3 , goli kipa huyo atakosa michezo 3 , msimu ujao katika mashindano hayo.
No comments: