Diego simeone, uso kwa uso na UEFA.
By Azizi Mtambo 15
Kocha wa klabu ya Athletico Madrid, Diego Simeone, amepewa adhabu ya mechi nne na shirikisho la UEFA, kwa kitendo chake kwenye mechi raundi ya kwanza nusu fainali ya Europa, na Arsenal.
Simeone, alionekana kumfokea mwamuzi baada ya mchezaji wa Arsenal, kutopewa kadi kwa faulo aliyoifanya ,mwamuzi akampa adhabu ya kwenda kukaa jukwaani.
Baada ya hapo akapata adhabu ya moja kwa moja ya mechi ambayo ndiyo mechi ya pili na Arsenal, kabla ya kesi yake kusikilzwa ,na sasa amepewa adhabu ya kufungiwa mechi nne kumaamisha atakosa mechi ya fainali dhidhi ya Marseille, itakayopigwa mwezi huu tarehe 16.
Pia kama watashinda fainali ina maansha atakosa super cup na mechi zilizobaki zitafidiwa kwenye mechi za makundi za msimu ujao.
No comments: