Ligi kuu England kuendelea kuendelea leo na michezo mbali mbali.
By Azizi Mtambo 15
Leo ikiwa Siku ya Jumapili, tarehe 6/05/2018, ligi kuu England kuendelea na michezo mbali mbali, huchezwa katika viwanja mbali mbali.
Mchezo wa kwanza utakuwa Manchester city, atakuwa nyumbani kumkaribisha Huddersfield, mchezo huo utapigwa majira ya saa 15:30 kwa saa za afrika mashariki mchezo utapigwa katika dimba la Etihad stadium, Manchester city mchezo wake wa mwisho alimfunga westham united mabao 4_1 katika dimba la Upton park mpaka sasa Manchester city, yupo nafasi ya kwanza akiwa na alama 93, huku Huddersfield, mchezo wake wa mwisho alimfunga Everton, mabao 2_0 katika uwanja wake wa nyumbani Amex stadium, Huddersfield yupo nafasi ya 16, akiwa na alama 35.
Mchezo unaofuatia utakuwa Arsenal atakuwa nyumbani kumkaribisha Burnley katika dimba la Fly Emirates, mchezo huo utapigwa majira ya saa 18:30 kwa saa za afrika mashariki ,Arsenal mchezo wake wa mwisho kwenye ligi kuu ,alipoteza mbele ya Manchester united, 2_1 katika dimba la Oldtraford, mpaka sasa Arsenal yupo nafasi ya 6 akiwa na alama 57, huku Burnley mchezo wake wa mwisho alitoa sare ya 0_0 na Brighton,Burnley yupo nafasi ya 7 akiwa na alama 57
Chelsea atakuwa nyumbani kumkaribisha Liverpool, katika dimba la Stamford bridge, mchezo huo utapigwa majira ya saa 18:30 kwa saa za afrika mashariki, mchezo wake wa mwisho kwenye ligi kuu alimfunga Swansea bao 1-0 katika dimba la liberty stadium, Chelsea yupo nafasi ya 5 akiwa na alama 66 huku ,Liverpool mchezo wake wa ligi kuu alitoa sare ya 0-0 na stoke city , katika uwanja wake wa nyumbani, Anfield, Liverpool yupo nafasi ya 3 akiwa na alama 72.
No comments: