Breaking

Fernando Toress, atapata furaha kubwa sana.

By Azizi-Mtambo 15

Mshambuliaji wa klabu yake Athletico Madrid, Fernando Toress, jana alionekana na furaha baada ya kuchukua nafasi ya Antonio Griezmani, kwenye mchezo wa fainali kombe la Europa, dhidhi ya Olympic Marseille, Toress, aliingia katika mchezo huo huku Athletico Madrid, wakiwa mbele kwa mabao 3-0.










Toress, alikuwa mshabiki mkubwa wa Athletico Madrid akiwa na umri wa miaka 5, alipata nafasi ya kujiunga na academic yao na mchezo wake wa kwanza alicheza mwaka 2001, akiwa na umri wa miaka 17.












Mwaka 2007,Toress alitangaza kuwa atajiunga na klabu ya Liverpool ya nchini uingereza, kwa kitita cha paundi million 20, mwaka 2010, wakati Athletico Madrid, wanatwaa ubingwa wa Europa anamfunga Fulham mabao 2-1 Toress, alikuwa Liverpool, pia wakati Athletico Madrid, wanatwaa mataji matano kwa kipindi cha miaka 2 na likiwemo kombe la ligi kuu Spain, mwaka 2014.












Toress, ameshinda kombe la uefa, FA cup, akiwa na klabu ya Chelsea,mwaka 2015, alirudi klabu yake ya Athletico Madrid, na hakufanikiwa kutwaa kombe lolote.








Msimu wa mwaka 2016, walingia fainali ya uefa dhidhi ya Real Madrid, walipoteza kwa mikwaju ya penalty na mshambuliaji huyo akiwemo ndani.












Msimu wa mwaka 2017/18, alifanikiwa kutwaa kombe lake la kwanza akiwa na Athletico Madrid, kwa kumfunga Olympic Marseille kwenye mchezo wa fainali baada ya mchezo huo kumalizika mshambuliaji huyo alionekana kuwa na furaha mkubwa mno.

No comments:

Powered by Blogger.