Breaking

Frank Ribery amwaga wino Bayern munch.

By Azizi Mtambo 15





Mshambuaji wa klabu ya Bayern munch, Frank Ribery, ameongeza mkataba mwaka wa mwaka moja na klabu hiyo utakao mfanya abaki klabuni hapo mpaka mwaka 2019, mshambhuliaji huyu mwenye umri wa miaka 35, mkataba wake wa hapo awali ulikuwa unafikia tamati mwisho wa msimu huu.












Ribery,mpaka sasa katika katika klabu hiyo amechezea michezo 305 katika mashindano yote na kufunga mabao 179,katika ligi kuu ya Ujerumani,amecheza michezo 247, na kufunga mabao 80 mpaka sasa.







Mpaka sasa, mchezaji huyo ametwaa makombe 15 kwa ngazi ya klabu .












Ametwaa kombe la ligi kuu ujerumani, maarufu kama bundesliga mara 8 , mwaka 2007/08, 2009/10, 2012/2013, 2013/2014, 2014/15, 2015/2016,2016/2017, na 2017/18,












Pia ametwaa kombe la uefa Mara moja mwaka 2012/13, ametwaa kombe la ujerumani mara 4 mwaka 2010/11, 2012/2013, 2016/17, 2017/18.












Pia ametwaa klabu bingwa ya dunia mara 1 mwaka 2014, mwaka 2012/13, alishinda tuzo ya mchezaji bora wa uefa.

No comments:

Powered by Blogger.