Mwamuzi huyu ndo atakayechezesha fainali ya uefa mwaka 2017/18
By Azizi Mtambo 15
Shirikisho la soka la UEFA, limemchagua mwamuzi kutoka nchini Serbia, Milorad Mazic, kuchezesha pambano la fainali ya Uefa, msimu huu mchezo huo utapigwa katika uwanja wa Nsc Olyimpisiky kyiev, nchini Ukraine, mchezo huo utapigwa tarehe 26 mwezi huu Mei 2018.
Liverpool, walifanikiwa kumtoa Asroma,kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 7-6, mchezo wa kwanza uliofanya katika uwanja wa Anfield,
Liverpool walibuka na ushindi wa mabao 5_2.huku mchezo wa pili uliofanyika katika uwanja wa Olympic mjijini Roma, wenyeji Arsoma walishinda 4_2 lakini walishindwa kuvuka hatua hiyo.
Real Madrid,alimtoa Bayern munch kwa kumfunga jumla ya mabao 4_3, mchezo wa kwanza uliofanyika katika dimba la Allianz Arena, real Madrid alipata ushindi wa mabao 2_1, na mchezo wa pili uliofanyika katika dimba la Santiago bernabeu, mchezo huo ulishia kwa droo ya 2_2.
Liverpool mpaka sasa wamechukua kombe hilo Mara 5 huku real Madrid, alichukua kombe hilo Mara 12 ndani ya msimu minne,real Madrid amecheza fainali Mara tatu.
Mwamuzi huyo kutoka Serbia pia alichezesha fainali ya kombe la dunia mwaka 2014, na pia alicheza fainali ya mashindano ya ulaya mwaka 2016.
No comments: