Harry kane huu ndo muda wa kufanya mabadiliko.
By Azizi-Mtambo 15
Harry Kane, moja ya washambuliaji bora kabisa duniani akiwa na umri wa miaka 24, Muingereza huyu anasifika kwa kutikisa nyavu akiwa uwanjani amechezea Tottenham, michezo 149, na kufunga mabao 109, katika michezo ya ligi kuu Uingereza, ana ufanizi mkubwa mno wa kufunga akiwa uwanjani na ni mkimya mno sana baadhi ya mabeki huwa wanapata tabu kumkabili mshambuliaji huyo ndo maana hata Rais, wa klabu ya Real Madrid, Fiorentina Perez, anamtolea macho na kumtaka ajiunge na miamba hiyo ya nchini Spain, huku akiamini umri wa Cristiano Ronaldo, unazidi kusonga mbele na kutokuwa hakuna mtu atakae kuwa anafunga mabao kwa ufanizi mkubwa.
Msimu wa mwaka 2015/16, alibuka kinara wa mabao katika ligi kuu Uingereza, akifunga mabao 25, na kutwa kiatu cha dhahabu msimu huo katika ligi kuu ,Tottenham, walimaliza nafasi ya 3 , wakiwa na alama 70, kuna utofauti mkubwa kati ya Harry, na timu anayochezea.
Msimu wa mwaka 2016/17, Muingereza, huyo alibuka tena mfungaji bora wa ligi kuu England, akiwa amefunga mabao 29, huku Tottenham, wakimaliza nafasi ya 2, kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 86, katika misimu yote msimu huo ndo walivuna alama nyingi zaidi Tottenham.
Msimu huu wa mwaka 2017/18, amemaliza nafasi ya pili nyuma ya mfungaji bora Mohamed Salah, Harry Kane, amefunga mabao 30, teyali kwenye ligi kuu Uingereza, hapo Jana umefikia tamati msimu huu wamemaliza nafasi ya 3, wakiwa na alama 77.
Pia amefunga mabao 30, kwa mara ya kwanza katika ligi kuu Uingereza, ndani ya msimu mmoja ndo tangu alivofanya ivo Kevin Phillips msimu wa mwaka 1999/2000.
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy, amesema kuwa kama kuna timu inamuhitaji mchezaji huyu waje na paundi million 200, ndo maongezi yanaanza sawa?inaweza ikawa nyingi au ndogo kwa klabu kama Real Madrid, kwa sababu mpira wa sasa hivi umekuwa na wigo mpana mikataba minono ya wachezaji , Tottenham washampiga pingu mchezaji huyo huku wakiamini Real Madrid, wanamtaka hudi na vumba, hapo turudi nyuma kidogo mwenyekiti huyo amekuwa mgumu kuuza wachezaji wake huku akitegemea mtu aje na pesa nzuri ndo maongezi yaanze, alimuulza Gareth bale msimu wa mwaka 2013/14, kwenda Real madrid kwa kitita cha paundi million 85, alimuuza Luka Modric kwenda Real Madrid kwa kitita cha paundi million 45, pia msimu huu kamuuza kyle walker kwenda Manchester city kwa kitita cha paundi milion 50, jinsi gani anajua kutengeneza fedha.
Ametuonesha kuwa Harry, anaweza kucheza la liga, kutokana na ubora wake wa kufunga huwa ajali timu imepata matokeo gani yeye anafunga tu.
Watu wengi wanaamini kuwa ligi kuu Uingereza, inaushindani zaidi na kwely?huu ndo muda wa Harry, kuondoka na kwenda kutafuta mafanikio na aache kumbukumbuku katika soka, tuzo anazo beba ni zake binafsi ,anahitaji msfanikio ya makombe zaidi
No comments: