Timu ya taifa ya italy yapata kocha mpya.
By Azizi-Mtambo 15
Roberto Mancini, amekubali kuwa mwalimu mpya wa Timu ya taifa Italy, akirithi nafasi ya Gian piera Ventura.
Mancini, amekubali kuwa kocha wa miaka miwili na mkataba wake utasainiwa rasmini hapo kesho.
Italy, imefeli kufuzu kombe la dunia, Mwaka huu na Ventura, akajitoa kwenye nafasi hiyo tangu hapo wamekuwa wakiangalia ni nani atakayeweza kuchukua mikoba hiyo.
Majina kama Carlo Ancelloti, na Antonio Conte, yalikuwa yakitajwa kama wenye nafasi kubwa ya kuchukua mikoba hiyo ya Italy.
Mancini, ndiye aliyeongoza Mancity, kubeba ubingwa wa Epl, mwaka 2012, pia aliipa Ngao ya hisani na kombe la FA,moja kwa miaka minne aliyokaa Etihad,kuanzia 2009_2013.
Juni 2007, Alijiunga na Zenit Saint Petersburg, ambapo Jana walivunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili.
No comments: