Lampard,Gerrad, Rio waionya real Madrid.
By Azizi Mtambo 15
Tukutane Kiev usiku wa Mei 26, Real Madrid jana usiku ilkuwa inasubiria itacheza na nani katika pambano la fainali kati ya Asroma na Liverpool huku real Madrid ikiwa ishatinga fainali kwa kuiondoa Bayern munch kwa jumla ya mabao 4_3 juzi jumanne katika dimba la bernabeu mjijini spaini.
Lakini mastaa watatu wa zamani wa England frank lampard , Steven Gerrad, na Rio Ferdinand , ambao kwa sasa ni wachambuzi mahiri nchini England na kuwa wamesema real Madrid kama inataka kombe hilo inahitaji ibadilike zaidi kuelekea mchezo huo.
Real Madrid imechukua taji hilo kwa Mara 12 lakini na kufika fainali yake ya tatu mfululizo ndani ya miaka minne bado mastaa hao ambao wote wamewahi kutwaa taji hilo wamedai Madrid ingeweza kutolewa na Bayern hapo juzi.
"Bayern walikuwa bora sana wote walikuwa katika hali yao na hakuna kitu kinachouma katika mpira kama kujua ulistahili kupata matokeo .real Madrid hii sio ile ya miaka michache iliyopita pamoja na mafanikio makubwa wanaweza kutegemea tenah bahati alisema lampard".
Kulikuwa na uwezekano wa Madrid kupambana na Liverpool ambayo Jana imefungwa mabao 4_2 na kuvuka kwa mabao ya ugenini jumla 7_6.
Nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard , ambaye alinyanyua taji hilo mwaka 2005 ,anaamini vijana hao wa jurgeon klopp watakwenda kyiev bila ya hofu baada ya kuiona safu ya ulinzi ya Madrid ikiwa ovyo.
" ni mafanikio ya juu sana kufika fainali tatu mfululizo, lakini ilikuwa ni wakati ambapo Madrid walikuwa na kiu sana.Bayern juzi walikuwa wametawala kila sehemu eneo la uwanjani ,nadhani watakuwa wanajuta walitawala mechi mbili zote na kukosa ubora sana alisema Gerrad ".
Beki wa zamani wa Manchester united Rio Ferdinand, alidai kuwa kama real Madrid itacheza fainali kama iliyocheza juzi itafungwa mno mjijini kyiev.
" kama watakwenda fainali na kucheza 4_4_2 kama walivofanya juzi watafungwa vibaya sana alisema Ferdinand".
No comments: