YANGA KUWAFUATA WARABU LEO.
By Azizi Mtambo 15
Kikosi cha Yanga, Leo Alhamisi kinatarajiwa kwenda Algeria,kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi kombe la shirikisho dhidi ya wenyeji wao USM Alger, huku Mghana akiwa mwamuzi wa kati.
Yanga ambayo kwenye michuano hiyo imepangiwa kundi D mechi yake ya kwanza ni dhidhi ya USM Alger, uwanja wa stade 5 juillet 1962, uliopo kwenye mji wa Algiers, Algeria.
Katika mchezo huo unaonza majira ya saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki, Mghana Daniel Nii Ayi Laryea , ndo atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo huo akisaidiana na Mnigeria ,Abel Baba pamoja na David laryeo, ambaye ni rai wa Ghana.
Akizungumza safari yao afisa wa habari wa Yanga, Dismas Ten,alisema
"Timu itaondoka leo(Alhamisi) hapa Dar-es-salaam , kupitia Dubai na kwenda moja kwa moja Algeria, tayari kwa mchezo huo.
" tulifahamu kwamba tuna mchezo huo kwa sababu ratiba ya CAF ililetwa mapema hivyo maandalizi ya sisi kwenda kupata matokeo mazuri na tuna imani kwamba tuna hatua nzuri zaidi.
Katika kundi hilo mbali na USM Alger pia Yanga imepangiwa na Rayon sport ya Rwanda, na Gor Mahia ya kutoka Kenya.
No comments: