LITAMBUE GWARIDE LA HESHIMA KWENYE SOKA.
By Azizi Mtambo 15
Guard of honour, kwa kingereza cha GB,na Guard of honour, kwa kingereza cha U.S.A.
Hili ni gwaride la heshima likitolewa kwenye sector nyingi tu ila sasa kwenye mpra gwaride la heshima utolewa kwa vigezo mbali mbali.
Moja ya gwaride, la heshima kwa mchezaji ambaye anafikia ukomo wa kutumikia club Fulani na alikuwa na mchango mkubwa tu kama sehemu ya team au kocha pia basi team husika kabla ya mchezo kuanza upewa guard of honour, kuagwa huo utaratibu upo.
Ukitaka kushuhudia hili basi mchezo wa Leo wa mwisho wa Arsene Wenger, kama kocha wa klabu ya Arsenal, atakuwa Emirates akiagwa.
Pia gwaride la heshima utolewa kwa team iliyofanikiwa kutwaa ubingwa na wanatoa heshima hiyo ni team zilizokuwa zinashiriki nae mashindano hayo basi gwaride la heshima litafanyika kwa team pinzani kujipanga mistari miwili na mabingwa kupita katikati wakipigiwa makofi.
Ila sasa guard of honour, sio lazima au team kufanya ustarabu na maamuzi binafsi kufanya hivo.
Miaka ya karibuni tumeshuhudia timu ambazo zinachukua kombe katika ligi zao zikiwa bado zina michezo kadhaa timu pinzani zinajipanga na kuwapa heshima kama bingwa wa ligi husika.
Kuelekea mchezo wa Leo wa El-classico, utakaopigwa Leo hapo baadae katika dimba la Nou camp, Barcelona, atakuwa nyumbani akiwa ameshatangzwa kuwa bingwa wa ligi kuu nchini Spain , atamkaribisha Real Madrid, ambaye yupo nafasi ya tatu katika ligi hiyo akiwa na alama71.
Nilimsikia kochwa wa real Madrid, kuelekea mchezo huu Zinedine zidane,akisema kuwa hawato wapigia makofi wapinzani kwa kutwaa ligi hiyo kwa sababu wao wakati wanatwaa ubingwa wa klabu bingwa ya dunia wapinzani wao hawaku wapigia makofi nikama sehemu ya heshma? Hapo lazima tujiulze wakati Real Madrid, anatwaa kombe hilo je? Barcelona, alishiriki mashindano hayo jibu linakuja hapana?
Me kwa mtazamo wangu naona Barcelona, walikuwa sahihi kufanya ivo kwa sababu ni mashindano ya nje ya spaini.
Lakini pia labda real Madrid, aliona ameonewa kwa sababu yeye ndo alijiona kama ndo aliyebaki mwakilishi wa kutoka nchi ya spaini, Madrid wanataka kulipa kisasi hicho.
Turudi nyuma kidogo mwaka 2008 , wakati real Madrid, wanatoa ubingwa wa Spain la liga ,klabu ya Barcelona ilijipanga na kuwapa heshma real Madrid huku wakiamini kwamba Madrid ametwaa ubingwa huo ndani ya Spain na sisi tukiwa tumeshiriki.
Leo hi Madrid, wameeka wazi kutowapigia makofi wapinzani wao na kuwapa heshima kuelekea mchezo huu.
Kuelekea mchezo huu, real Madrid kwa mtazamo wangu hawapo sahihi kabisa kwa nin?usijipange kuwapa heshima kuelekea mchezo huo.
No comments: