Ligi kuu England kuendelea leo na michezo mbali mbali
By Azizi Mtambo 15
Leo ni tarehe 09/05/2018, ligi kuu England, kuendelea na michezo mbali mbali kutumia vumbi katika viwanja mbali mbali.
Chelsea vs Huddersfield, Chelsea atakuwa katika dimba lake la Stamford bridge kumkaribisha Huddersfield, mchezo huo utapigwa majira ya saa 21:45 kwa saa za afrika mashariki, Chelsea, mchezo wake wa mwisho alishinda bao 1-0 dhidhi ya Liverpool katika uwanja wake wa nyumbani mpaka sasa Chelsea yupo nafasi ya tano akiwa na alama 69, anahitaji kushinda mchezo huu ili hajiekee nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa msimu ujao, Huddersfield mchezo wake wa mwisho alitoa sare 0_0 na Manchester city, katika dimba la Etihad stadium, mpaka sasa yupo nafasi ya 16 , akiwa 36, anahitaji ashinde ili ajihakikishie kubaki ligi kuu msimu ujao.
Leicester city vs Arsenal, Leicester atakuwa nyumbani kumualika Arsenal, mchezo huo utapigwa katika dimba la king power stadium, mchezo huo utapigwa saa 21:45 kwa saa za afrika mashariki, mchezo wa mwisho Leicester city, alifungwa katika dimba lake la nyumbani mabao 2-0 na westham united, mpaka sasa yupo nafasi ya 9 na alama 44, ayupo katika nafasi ya kushika daraja. Arsenal , mchezo wake wa mwisho alimfunga Burnley, mabao 5_0 katika uwanja wake wa nyumbani, mpaka sasa Arsenal wapo nafasi ya sita wakiwa na alama 60 na ashapoteza nafasi ya kucheza uefa msimu ujao.
Manchester city vs Brighton, mchezo huo utapigwa katika dimba la Etihad stadium, Manchester city atakuwa katika uwanja wake wa nyumbani, mchezo wao wa mwisho walitoa sare ya 0-0 dhidhi ya Huddersfield field, city mpaka sasa ashatangazwa kuwa bingwa mpya wa msimu wa mwaka 2017/18 , akiwa na nafasi ya kwanza na alama 94, brighton, mchezo wake wa mwisho alimfunga Manchester united, bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani, Falmer stadium, mpaka sasa yupo nafasi ya 14 na alama 40.
Tottenham vs Newcastle, mchezo huo utapigwa katika dimba la Wembley stadium, Tottenham atamkaribisha Newcastle mchezo huo saa 22:00 kwa saa za afrika mashariki, Tottenham mchezo wake wa mwisho alimfunga na westbromic Albion bao 1-0 , mchezo huo uliopigwa katika dimba la Hawathrow park, mpaka sasa Tottenham yupo nafasi ya 4 na alama 71, newcastle, mchezo wake wa mwisho alimfunga Watford, mabao 2-0 ,katika uwanja wa Vicarage Road, newscatle akiwa nafasi ya 10 ,na alama 41.
No comments: