Ligi kuu England kutimua vumbi leo.
By Azizi Mtambo 15
Ligi kuu England, kuendelea Leo tarehe 05/05/2018, michezo ya ligi kuu England, kuendelea katika viwanja mbali mbali.
Stoke city vs Crystal palace, mchezo huo utapgwa majira ya saa 14:30 kwa saa za afrika mashariki, stoke city, atakuwa nyumbani kumkaribisha Crystal palace katika dimba la Britannia stadium,. Mchezo wa mwisho stoke city aliweza kutoa droo na Liverpool ya 0-0 mpaka sasa akiwa na nafasi ya 19, na alama 30, huku crystal palace mchezo wake wa mwisho uliofanyika king power aliweza kumfunga Leicester city mabao 5-0 mpaka sasa Crystal palace yupo nafasi ya 12 akiwa na alama 38.
Mchezo wa pili utakuwa Bournemouth vs Swansea city mchezo huo utapgwa mishale ya saa 17:00 jioni kwa masaa za afrika mashariki ambapo Bournemouth atakuwa nyumbani katika uwanja wa vitality stadium akimkarbisha Swansea city, Bournemouth mchezo wake wa mwisho alifungwa na Southampton mabao 2-1 katika uwanja wa st marys park Bournemouth akiwa na nafasi ya 13 akiwa na alama 38, huku Swansea city mchezo wake wa mwisho uliofanyika katika dimba la nyumbani liberty stadium, alifungwa bao 1-0 na Chelsea, mpaka sasa Swansea , yupo nafasi ya 17 akiwa na alama 33.
Mchezo mwengine utapigwa majira ya saa 17:00 kwa saa za afrika mashariki Leicester city, atakuwa nyumbani katika uwanja wake wa king power kumkaribisha westham united , mchezo wa mwisho Leicester city alikubali kipigo cha mabao 5_0 kutoka kwa Crystal palace, Leicester city yupo nafasi ya 9, akiwa na alama 44, westham united mchezo wake wa mwisho alifungwa mabao 4_1 na Manchester city , mpaka sasa westham akiwa nafasi ya 15 , na alama 35.
Mchezo mwengine utakuwa kati ya Watford vs Newcastle united, mchezo huo utapigwa majira ya saa 17:00 kwa saa za afrika mashariki Watford atakuwa katika uwanja wake wa nyumbani vicarage road kumkaribisha newscatle united, Watford , mchezo wake wa mwisho alifungwa na Tottenham mabao 2-0 katika uwanja wa Wembley , mpaka sasa Watford yupo nafasi ya 14 , akiwa na alama 38, Newcastle mchezo wake wa mwisho alkuwa nyumbani katika dimba la St James park kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa westbromic Albion, mpaka sasa Newcastle yupo nafasi ya 15 akiwa na alama 35.
Westbromic vs Tottenham , atakuwa nyumbani westbromic, katika dimba la Hawthrow park, westbromic alishinda mchezo wake wa mwisho bao 1-0 dhidhi ya Newcastle , katika dimba la st James park, westbromic akiwa nafasi ya 20 ana alama 28, huku Tottenham, mchezo wake wa mwisho alimfunga Watford, katika uwanja wa Wembley ,Tottenham akiwa nafasi ya 4 na alama 71.
Everton vs Southampton mchezo huo utakuwa wa mwisho utapigwa majira ya saa19:30 kwa saa za afrika mashariki Everton ,atakuwa nyumbani katika dimba la Goodson park , kumkaribisha Southampton, mchezo wake wa mwisho Everton ,alishinda mabao 2-0 dhidhi ya Huddersfield, katika dimba la Amex stadium, Everton akiwa nafasi ya 8 na alama 48, huku Southampton, mchezo wake wa mwisho alimfunga Bournemouth mabao 2-1 katika uwanja wa st Mary's park , Southampton, yupo nafasi ya 18 akiwa na alama 32.
No comments: