Breaking

Yahya Toure kuwaaga Manchester city.

By Azizi Mtambo 15

Kocha wa klabu ya Manchester city Pep Guardiola, Leo ame fanya mahojiana na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa ligi kuu England dhidhi ya Huddersfield.

Lakini pia ameongelea hatma ya kiungo wake Yaya Toure, na kusema kuwa mwisho wa msimu huu ataondoka klabuni hapo.


Pep, akisema kuwa mchezaji huyo watamtumia kwenye michezo yao ya mwisho ni kama sehemu ya kumuaga na kumpa nafasi hiyo msimu huu yaya ametumika kama mchezaji wa akiba na klabu hiyo.

Toure ,alijiunga na klabu hiyo mwaka 2010 akitokea klabu ya Barcelona ya nchini Spain, amecheza michezo 229 na kufunga mabao 59 na klabu hiyo.

Ameshinda makombe 7 ndani ya miaka 8 aliyedumu klabuni hapo ameshinda kombe la ligi mara 3 ikiwemo mwaka 2012,2014,2018, pia ameshinda kombe la FA cup mara 1 mwaka 2011, na pia kombe la capital one mara 3 ikiwemo mwaka 2014,2016,2018.



Pia ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa afrika mara 4 mfululizo mwaka 2011,2012,2013,na 2014.

No comments:

Powered by Blogger.