Breaking

Mwakyembe atoa pongezi kwa TBC na KWESE SPORT.

By Azizi-Mtambo 15



Waziri wa habari sanaa utamaduni na michezo nchini Dkt.Harrison Mwakyembe,amewapongeza TBC na TV one kwa kufanikisha kuonyesha mechi 32 za kombe la dunia bure kabisa.












Mwakyembe,amesema kufurahishwa na uamuzi wa vituo hivyo vya runinga kuamua kuonesha mashindano hayo yatakayoanza mwezi juni 2018, huko Urusi.












Mbali na hayo, waziri huyo mwenye dhamana ya michezo amevipongeza kwa kuonesha uzalendo kwa watanzania, wanaosubiri burudani hiyo kwa hamu ambapo wataweza kutazama mechi hizo bure.












"Nimefurahishwa na uzalendo wa TBC na TV one, kwa kuwapatia burudani watanzania bure.hivyo itasaidia pia televisheni hizo kujitangaza kimataifa na kupata matangazo",













Aliongeza " hivyo ni fursa kwa watanzania, sasa kupata ya bure kupitia muunganiko wa televisheni hizo mbili za TBC na TV one, alisema Mwakyembe, katika ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia.

No comments:

Powered by Blogger.