shirikisho la soka duniani FIFA yataja waamuzi 99, kuelekea michuano hiyo.
By Azizi-Mtambo 15
Shirikisho la soka Duniani FIFA, limechaguwa marefa 36, na waamuzi wasaidizi 63, kutoka nchini 46, mbali mbali kuelekea michuano hiyo itakayo anza mwezi ujao nchini Urusi.
Katika orodha ya waamuzi waliochaguliwa jumla ni 99, wengine kati hao watahusika katika teknolojia ya video Assistant referee, na wengine watakuwa waamuzi wa kati na wengine watakuwa wasaidizi.
Uchaguzi wa waamuzi hawo walikuwa wana angalia vigezo ambavyo kama waamuzi hao wamekidhi vigezo mbali mbali kama, ujuzi, utu, na uwezo wa kuelewa Mpira kwa kina na uwezo wa kuelewa mchezo wa mpira wa miguu na matukio ya uwanjani mbinu zilizotumiwa na timu zote zikiwa uwanjani.
Kwa kipindi cha miaka 3, iliyopita kulikuwa na semina mbali mbali zimekuwa zikitolewa kwa waamuzi hao kwa kina katika mchezo wa kiungwana(fair play) ulinzi kwa wachezaji na taswira ya mchezo na uendelevu wa kanuni za uwanjani.
No comments: