Breaking

Steven Gerrad akubali kujiunga na Rangers ya Scotland.

By Azizi Mtambo 15







Nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool, na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard , amekubali kwenda kuwa kocha mpya wa Rangers, ambayo inashirika ligi kuu Scotland.





Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 amekubali kusaini mkataba wa miaka 4 na klabu hiyo kwa taarifa kutoka mtandao wa sky sport mjijini England.






Gerrard , Leo hii amewasili mjijini, Glasglow, na kusaini mkataba huo wa miaka 4 kuiona klabu hiyo na atakuwa msaidizi wake Gary McAllister,.






Gerrard mwenye umri wa miaka 37, amekuwa katika academy ya Liverpool akiwa kocha wa vijana kwa ngazi ya klabu toka mwezi 4 mwaka Jana.




Gerrard aliyecheza Liverpool michezo 504 na kufunga mabao 120 katika mashindano yake yote kipindi hakiwa na klabu hiyo.



Pia amecheza timu ya taifa ya England, michezo 114 na kufunga mabao 21.


Rangers mpaka sasa wakiwa nafasi ya 3 katika ligi kuu Scotland, wakiwa nyuma ya point 13 na kinara wa ligi hiyo Celtics.

No comments:

Powered by Blogger.