Zidane, acheza na nyakati za Real Madrid.
By Azizi -Mtambo 15
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane, amezaliwa Tarehe 23/June/1972, akiwa na umri wa Miaka 45, ametangaza kujiuzulu ghafla kuifundisha klabu hiyo wakati Mkataba wake ulikuwa unaisha Mwaka 2020, kwa maana hiyo Zidane, amelipa fidia kwa kuvunja Mkataba huo.
Zidane, alianza kuifundisha Real Madrid, B na kupandishwa katika timu kubwa na kuwa kocha msaidizi chini ya Muitaliano Carlo Ancelloti, Msimu wa Mwaka 2014/15, alijifunza mengi mno kupitia kocha huyo Muitaliano na walishinda champion ligi baada ya kukaa takribani Miaka 12 bila ya taji hilo tukumbuke mara ya mwisho Real Madrid, walitwa ubingwa huo Mwaka 2002 ilikuwa chini ya Spain, Vicente Del Bosque, pia zidane, alifunga bao muhimu katika mchezo huo na kumaliza kwa mabao 2-1, fainali hiyo ilipigwa Mjiini Glasgow Scotland.
Msimu unaofuata katikati Rafael Benitez, alifutwa kazi na kibarua akapewa Zidane, ulikuwa msimu wa Mwaka 2015/16, watu wengi walijaji na kusema Zidane, kapewa timu Kubwa akiwa ana hata uzoefu na timu hiyo?pengine jibu ni rahisi mno Zidane, alisoma nyakati na kutembelea ufalme wa Ancelloti, msimu wake wa Kwanza alitwa champion league na watu wengi hawakuamini huku akisema kuwa amebatisha zaidi watu walisema wapewe mda zaidi waone ubora wake?
Zidane,msimu unaofuata 2016/17,alimpandisha Casemiro, na kumpa nafasi katika mchezo mkubwa duniani El classico, kupambana na watu kama Iniesta, Bosquet, eneo la kiungo mchezo huo uliishia kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.alipoulizwa kuwa kwa nin umempa Casemiro, nafasi katika mchezo mkubwa kama huu Zidane, alijibu kuwa nilimuamini na uwezo wake wa hali ya juu kukaba?tuache hayo Msimu huo pia alitengeneza rekodi ya kushinda champion ligi kwa mara ya pili mfululizo, na kutengeneza rekodi ya kuwa kocha wa Kwanza kufanya ivo? Je pia unajua Zidane, ndio kocha ambae ajafungwa na Barcelona, nyumbani na ugenini.
Alitengeneza timu yake eneo la kiungo uwiano wa Luka Modric, Toni Kroos,na Casemiro, alipendelea mfumo wa 4-3-3 huku akitegemea sehemu Kubwa ya kiungo kuanzisha mashambulizi na alifanikiwa hicho kitu.
Zidane, huu msimu alikuwa amehusishwa sana kufukuzwa baada ya kupata matokeo mabovu kwenye ligi kuu nchini Spain, alipewa mchezo wake wa Mwisho wa Uefa ilikuwa dhidi ya Psq, hatua ya 16 bora na kufanikiwa kuwatoa pengine? Baada ya kuwapa Madrid, uefa kibarua chake kilikuwa na unafuu kidogo?Zidane ndo kocha wa Kwanza kuchukua Uefa mara tatu mfululizo? amejenga historia ambayo itadumu kwa miaka mingi Sana?
Zidane ameiongoza Real Madrid, msimu mitatu na kutoa mataji 9 ya kiwemo.
Uefa mara 3.
Uefa super Cup mara 2.
la liga mara 1.
Klabu bingwa ya dunia mara 2.
Spanish super Cup mara 1.
Pia ameiongoza Real Madrid, michezo.
Michezo. Ushindi . Mabao .wastani win
149. 104. 393. 69.8.
Zidane, ameiacha Real Madrid, kwa sababu ukiangalia kizazi cha timu hiyo kinaanza kupotea kwa sababu ya umri kuanza kuwatupa mkono ukiangalia wachezaji wanaonza kwenye kikosi hicho.
Kama nahodha wao Sergio Ramos ana umri wa miaka 32, Cristiano Ronaldo, ana umri wa miaka 33, Luka Modric, ana umri wa miaka 32, Marcelo Viera, ana umri wa miaka 30, Gareth Bale, Isco, wanahushishwa kuondoka klabuni hapo ameona kwamba kizazi kilichompa mafanikio kwa muda mfupi kinapotea ameogopa aibu ambayo lbda ingemkuta na kuharibu sifa yake? Zidane, alicheza na akiri ya Perez.
Baada ya kutangaza kujiuzulu haya ndo maneno aliyosema Rais wa Real Madrid, Fiorentina Perez, "uamuzi wa Zidane, ulikuwa wa ghafla Hakuna ambaye alikuwa anajiandaa mpaka sasa hatujajua nani atamrithi.
Zidane, amekuwa ndo kocha wa Kwanza kwenye historia ya Fiorentina, kuondoka bila ya kufukuzwa.
Tusikie sasa maneno ya Zidane, baada ya kuchukua uamuzi huo.
"ameeleza kuwa kila kitu kinahitaji mabadiliko hivyo ni wakati wa mtu mwingine kuingoza klabu hiyo yenye historia Kubwa nchini Spain, na Ulaya,
"akisema timu iendelee na ipambane huku akisisitiza anaipenda Madrid.
Zidane, ameogopa huenda rekodi yake ingeharibika msimu ujao au angekutana na aibu kubwa mno. Kizazi cha Real Madrid, kilichotwaa ubingwa wa uefa Mwaka 2002, kilipotea na kuja kizazi kingine ambacho kilitwaa ubingwa huo Mwaka 2014.
No comments: