Breaking

Tuangalie sehemu ya nne kiwanja kitakacho tumika kuelekea michuano ya kombe la dunia.

By Azizi -Mtambo 15


Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea michuano ya kombe la dunia  itakayo fanyika nchini Urusi.

Shirikisho la soka duniani  FIFA,  limechagua viwanja 12 vitakavo tumika kuelekea michuano ya kombe la dunia. basi leo tunaangalia kiwanja namba nne kinaitwa.

Mordovia Arena, hichi ni moja ya kiwanja kinacho patikana nchini Urusi, kitakacho tumiwa kuchezea baadhi ya michezo.kiwanja hicho  kipo karibia na mjiji mkuu wa Saranka.

Ndo uwanja mdogo ambayo michuano hiyo itafanyika ambao ni Mordovia Area Saransk. Sarank ni mji mkuu ambao una idadi ya watu wapatao 307000 , pia uwanja huo umejengwa karibia na mto wa Insar,  ambao unaenda mpaka Sarank.


Uwanja huo unaingiza watu wapatao 44,000 pia walio design uwanja huo ni kampuni ya New stadium,  pia ume desiginiwa Kama shape ya yai pia una rangi Kama zifuatazo Nyeupe, Njano,  na ya machungwa kwa mbali. Pia umetumia kiasi cha ujenzi ni kitita cha Euro million 300.

Uwanja huo umejengwa Mwaka 2010, na kufanyia marekebisho Mwaka 2018, kuelekea michuano ya kombe la dunia.


Mchezo wa Kwanza katika uwanja huo ulichezeka kati ya Local side FC dhidi ya Mordovia,  na kumalizika sare ya 0-0.

Kuelekea michuano ya kombe la dunia mchezo wa ufunguzi kwenye uwanja huo utakuwa kati ya.

Den Mark

Vs

Peru.

Mchezo huo utapigwa Juni 16.

Colombia

Vs

Japan.

Mchezo huo utapigwa Juni 19.

Iran

Vs

Portugal.

Mchezo huo utapigwa Juni 25.

Panama

Vs

Tunisia.

Mchezo huo utapigwa Juni 28.

Hiyo ndo baadhi ya michezo itakayo pigwa kwenye uwanja huo.

Baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika FC Mordovia,  watarudi kutumia uwanja wao katika mchezo ya ligi kuu Urusi.

No comments:

Powered by Blogger.