Tuangalie sehemu ya tatu ya uwanja utakao tumika kuelekea michuano ya kombe la dunia.
By Azizi -Mtambo 15
Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea michuano ya kombe la dunia itakayo fanyika nchini Urusi.
Shirikisho la soka duniani FIFA, limechagua viwanja 12 vitakavo tumika kuelekea michuano hi na mechi zitachezeka katika viwanja hivo.
Basi leo tuangalie kiwanja kinachoitwa.
Rostov Arena, ni moja ya kiwanja kinacho patikana nchini Urusi, kiwanja hichi kipo karibu na mto wa Doni, kimejengwa Mwaka 2018, kuelekea michuano ya kombe la dunia.
Kiwanja hicho kilifunguliwa Mwaka 2018, Tarehe 15/04/2018, mchezo wa Kwanza ulipigwa kati ya Rostov, dhidi ya Khabarousk.
Uwanja huo unamilikiwa na FC Rostov, inayo shiriki ligi kuu ya Urusi, kinaingiza idadi ya mashabiki takribani 45,000 .
Kuelekea michuano ya kombe la dunia zitapigwa mechi nne za makundi na hatua ya 16 bora.
Mechi ya Kwanza itapigwa kati ya Brazil dhidi ya Switzerland, na mshindi katika kundi G, atacheza na mshindi wa kundi H, katika hatua ya 16 bora.
Mechi zengine ambazo zitachezeka katika uwanja huo Kama ifuatavyo.
Uruguay
Vs
Saudia Arabia.
Mchezo huo utapigwa Juni 20.
Korea Republic
Vs
Mexico.
Mchezo huo utapigwa Juni 23.
Iceland
Vs
Croatia.
Mchezo huo utapigwa Juni 26.
Uwanja huo upo karibia na stesheni za barabara za treni kama kilometer nne kutoka uwanjani.
Pia kuna hotel karibia na mto ambao upo karibu na uwanja pia upo karibu na hotel Goleboya Volna, Vysokii, Bereg park hotel, na Luxurious hotel petrovsky.
No comments: