Breaking

Tuangalie sehemu ya Saba Kiwanja kitakacho tumika kwenye michuano ya kombe la dunia.




By Azizi -Mtambo 15.

Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea michuano ya kombe la dunia itakayo fanyika nchini Urusi.

Shirikisho la Soka duniani FIFA,  limechagua viwanja 12 vitakavotumika kuelekea michuano hiyo.leo tunaendelea na uchambuzi wetu wa Kiwanja cha Saba kukichambua.

Samora Stadium,  ni moja ya kiwanja kinachopatikana kule nchini Urusi,  kimejengwa Mwaka 1586, uwanja huo unaingiza idadi ya watu takribani 45,000 uwanja huo upo sehemu inaitwa Samara,  mkoa huo una watu wapatao million 1.5.

Baada ya michuano ya kombe la dunia kumalizika uwanja huo utatumiwa na klabu iliyopanda daraja msimu huu inaitwa Krylia Sovaton , utakuwa unachezea mechi zake za nyumbani kwenye uwanja huo.

Uwanja huo ulifunguliwa tarehe 28/04/2018, mchezo wa Kwanza ulicheza kati ya Krylia, dhidi ya Fakel Voronezh,  mchezo huo ulimalizika kwa Krylia,  kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mchezo wa pili tena ulipigwa katika uwanja huo uliingiza Idadi ya watu wapatao 40,000  mchezo huo ulikuwa kati ya Krylia dhidi ya Kaban Krosnodar.

Uwanja huo pia ulifanyiwa marekebisho na shirikisho la soka duniani FIFA,ndani ya Mwaka 2018. Kuelekea michuano hii.

Ujenzi wa uwanja huo ulitumia Dolla za kimarekani,  million 320.

Kuelekea michuano ya kombe la dunia kwenye uwanja huo zitapigwa mechi nne za makundi,  16 bora na robo fainali.

Tuangalie baadhi za mechi zitakazo pigwa kwenye uwanja huo.

Costa Rica

Vs

Serbia.

Mchezo huo utaopigwa Juni 17.

DenMark

Vs

Australia.

Mchezo huo utapigwa Juni 21.

Uruguay

Vs

Urusi.

Mchezo huo utapigwa Juni 25.

Senegal

Vs

Colombia.

Mchezo huo utapigwa Juni 28.

Na mechi za 16 bora na robo fainali.

No comments:

Powered by Blogger.