Breaking

Tufahamu kiwanja cha kumi kitakachotumika kwenye fainali za kombe la dunia.

By Azizi -Mtambo 15.

Zikiwa zimebakia siku kadhaa kuelekea fainali za kombe la dunia zitakazo fanyika nchini Urusi.

Leo tunachambua kiwanja cha kumi kitakachotumika kwenye fainali hizo.

Kaliningrad Stadium  kiwanja hichi kinapatikana nchini Urusi,  kilijengwa Mwaka 2015, na kufunguliwa Mwaka 2018, kilifunguliwa Tarehe 11 Mwezi wa nne mechi ya Kwanza ilikuwa kati ya Baltika dhidi ya Krylia Soveton,  mchezo huo ulimalizika kwa Baltika,  kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Uwanja huo unaingiza idadi ya watu wapatao takribani 35,000 uwanja huo upo katika eneo linaloitwa Oktya Brsky Island.

Baada ya fainali za kombe la dunia uwanja huo utatumiwa na timu ambayo inashiriki ligi kuu Urusi, ambayo inaitwa FC Baltika,  katika michezo yake ya nyumbani.

Kuelekea michuano ya kombe la dunia uwanja huo zitachezwa michezo nne ya makundi.

Croatia

Vs

Nigeria.

Serbia

Vs

Switzerland.

Spain

Vs

Morocco.

England

Vs

Belgium.

No comments:

Powered by Blogger.