Breaking

Tufahamu mambo haya kuelekea mchezo wa Portugal, dhidi ya Morocco.

By Azizi -Mtambo 15.

Leo siku ya Jumatano fainali za kombe la dunia kutakuwa na mchezo wa Kwanza wa kundi B kati ya Portugal, dhidi ya Morocco,  mchezo huo utapigwa saa tisa kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki. Pia utapigwa katika dimba la Luzhinik Stadium.

Kwa taarifa kwa timu zote mbili.

Portugal, leo anashuka dimbani kutafuta ushindi baada ya mchezo wao wa Kwanza kutoa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Spain. huku nyota wao Cristiano Ronaldo,  akifunga hatrick yake ya 51 katika maisha yake ya soka.

Portugal,  wanamini kuwa safu yao ya ulinzi itacheza vizuri tofauti na mchezo wao wa Kwanza waliruhusu mabao matatu.katika safu ya ulinzi leo itaongozwa na Bruno Alves,  na Jose Fonte,  huku beki wao Jorge Santos,  akiwa bado majeruhi.

Kocha wa Portugal,  Fernando Santos,  amesema kuwa anafurahi kuona kiwango cha nyota wake Ronaldo,  akicheza juu ya kiwango.

"tunaenda kucheza na Morocco,  naamini Ronaldo,  atacheza mechi yake kubwa na tumejipanga zaidi kwenye mchezo wa leo",.


"Portugal,  walikuwa Mabingwa wa Ulaya,  kwa sababu Ronaldo,  alikuwa nahodha wa timu hiyo.



Morocco,  watamkosa mabeki wao Nordin Amrabat,  na Nabil Dirar,  hawawezi kucheza mchezo huo.



Kocha wa Morocco,  Herve Renard,  amesema kuwa kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Portugal,  itakuwa ngumu mno kumzuia Ronaldo, hata kama ukitaji upate sare unahitaji uweke mikakati kuhusu Ronaldo.


"hata kama akimuekea Ronaldo,  akabwe na watu watatu na wachezaji wengine wa Portugal, watakabwa na nani.


"wana washambuliaji wengi ambao wanaweza kucheza vizuri na wao ni mabingwa wa Ulaya,".


Tukumbuke.

Mara ya mwisho Morocco,  na Portugal,  kukutana katika fainali za kombe la dunia ilikuwa Mwaka 1986, kule nchini Mexico.


Vikosi vinavoweza kuanza leo.

Portugal.  Patricio,  Cedric,  Pepe,  B. Alves, Guerrero,  William,  Mountinho,  B Silva,  Mario,  Andre Silva,  Cristiano Ronaldo.

Morocco. El Kajoui,  Hakimi,  Saiss,  Benatia,  Mendyl,  El Ahmadi,  Ziyach,  Boussoufc,  Belhando,  Amrabat,  Boutaib.

No comments:

Powered by Blogger.