Uchambuzi mechi kati ya Colombia, dhidi ya Japan.
By Azizi-Mtambo 15.
Leo jumanne kutakuwa na mechi ya mapema itakayochezwa saa tisa kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki kati ya Colombia, dhidi ya Japan, mchezo huo utapigwa katika dimba la Mordovia Arena.
Mchezo huo wa Kundi H.
Colombia, wamerika kusini, kwenye fainali za kombe la dunia Mwaka 2014, walitolewa hatua ya robo fainali dhidi ya Brazil, kwa kufungwa mabao 2-1.
Nyota wa Colombia, James Rodriguez, pia fainali hizo aliibuka mfungaji bora za Mwaka 2014, huenda asianze mchezo wa Leo baada ya kupata majeraha ya misuli na akiwemo kiungo wao Wilmar Barriors.
Kocha wa Colombia, Jose Peckerman, akisema kuwa hasaivi mpira umebadilika wachezaji na tuna timu bora nafikiri na ina nguvu.
Japan, walipoteza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Ghana, na Switzerland.
Kocha wa Japan, Akira Nishino, toka amechukua timu hiyo ameiongoza michezo mitatu toka alivopewa Mwezi wa nne.
Japan, wachezaji wao wawili ambao walikuwa majeruhi wamerudi kikosini ambao Shinji Kagawa, na Keisuke Honda, huku kiungo wao anachezea Leicester City, Shinji Okazaki, bado anaumwa maumivu ya nyonga.
Kumbukumbu Colombia, mara ya mwisho alimfunga Japan, mabao 4-1 katika fainali za kombe la dunia Mwaka 2014, huku nyota wa Colombia, James Rodriguez, akifunga mabao mawili.
Vikosi vinavoweza kuanza leo.
Colombia, Ospina, Arias, Mina, D. Sanchez, Mojica, Uribe, Aguilar, C. Sanchez, Cuadrado, Bacco, Falcao.
Japan. Kawashima, Endo, Yoshinda, Nagatoma, Sakai, Shibasaki, Yamaguchi, Muto, Kagawa, Inui, Osako.
No comments: